Na. MED News: 4/9/2017
Wahenga walisema "Penye nia pana njia" Msemo huu ni wa kale japo unaishi hadi sasa. Kila unapotia nia katika jambo fulani mafanikio yake utayapata mara wakati wake utakapo wadia. Jambo muhimu hapa ni kutokukata tamaa na kulisimamia vyema lile unalotaka likuletee maendeleo.
Kijana Sefu mwenye bukta pichani alianza kutia nia katika kipaji chake cha sanaa tangu akiwa shule ya Msingi; hakuona shida kutumia kila fursa aliyoipata katika kuendeleza kipaji chake cha sanaa ya uigizaji na vichekesho. Hakujali malipo au kutunzwa; vyovyote iwavyo yeye aliamini katika kuwa msanii. Alitambua kuwa ana kipaji ambacho anapaswa kukitolea jasho ili siku moja kimlipe.
Msanii Seff akiigiza katika Mahafali ya Darasa la
Saba katika Shule ya Msingi Chidachi -2015
|
Sefu alitumia mwendo wa kilometa tano kwa siku kwenda na kurudi shuleni yeye hakujali, kila alipopita alitumia mwanya huo kuonyesha kipaji chake cha sanaa. Hakukata tamaa kwa umbali wa makazi na iliko shule; alikaza mwendo ili ahitimu kidato cha nne katika shule yake ya sekondari Kikuyu.
Alitambua thamani ya sanaa yake si uwezo wa kuigia pekee bali ELIMU na maarifa yanayoendana na mabadiliko makubwa ya sayansi na teknolojia duniani. Alitambua kuwa sanaa bila Elimu haitadumu; aliwaza kuwa msanii nje ya Dodoma, nje ya Tanzania na hata nje ya Afrika Mashariki, Afrika ya kati nk.
Baada ya mihagaiko kijana Sefu mwaka huu 2017 anatarajia kuhitimu elimu yake ya sanaa katika Chuo cha Sanaa Bagamoyo! Atakuwa msanii, atakuwa msanii msomi; atakayetumia kipaji chake cha kuzaliwa, elimu yake ya darasani na mafunzo ya sanaa aliyoyapata katika Chuo cha sanaa Bagamoyo kusongeza karibu ndoto yake ya mafanikio katika sanaa.
Malengo ya Seff ni changamoto kwa vijana ambao mara tu wanapojigundua kuwa wana uwezo wa kucheza muziki, kucheza show kwenye harusi, kipaimara na sherehe mbalimbali; hudharau elimu na kujikita kwenye sanaa ambayo hudumu kwa muda mfupi na kukuacha katika cangamoto.
Pongezi kwa kijana Seff na vijana wote wanaotambua vipawa vyao na kuvipa nafasi pasi na kuacha kuendelea na masomo katika shule za msingi na sekondari Elimu ni mwanga utakao angaza katika vipaji, vipawa na ndoto zako zote! Tutakuunga mkono mara tu urejeapo Dodoma. Big Up Seff.
UKIITUMIA VYEMA SANAA NI AJIRA KWAKO
Reviewed by Unknown
on
October 04, 2017
Rating:
No comments: