HALI DUNI ISIKUKATISHE TAMAA KATIKA ELIMU.


Na. MED News 
Usiikubali hali yako ya sasa; hangaikia kesho yako!
Ni jambo la kawaida katika jamii kuona au kuishi na watu wenye hali tofauti katika kkipato. Hali ya kipato katika jamii nayo imekuwa ikijadiliwa na wengi ikidaiwa kuwa ni kikwazo aktika kupata elimu (hasa katika kugharamia) mahitaji ya shule nk.

Kutumia hali duni katika familia kama kikwazo muhimu katika kupata elimu ni moja kati ya makosa makubwa tunayoyafanya na kuwakatishia watoto wetu ndoto zao za mafanikio. Bila kujali hali ya kiuchmi katika familia tunapaswa kuidhamini elimu kwa kila namna.

Katika picha hii tunaweza kuona hali ilivyo kwa baadhi ya wanafunzi katika shule zetu ama za msingi na hata zile za sekondari. Haijalishi ni sekondari ya umma au ni binafsi bali muhimu hapa ni kuwa huyu naye ni mwanafunzi.

Wanafunzi aina hii wako kwenye jamii zetu, ni majirani zetu, ni watoto wa ndugu zetu, ni watoto wa marafiki zetu nk.

Suala la uwajibikaji wa jamii katika kuwezesha upatikanaji wa mazingira rafiki ya kujifunzia ni suala la msingi sana kwetu. Mara kadhaa kumekuwa na malalamiko juu ya miundombinu ya shule, vifaa vya kujifunzia nk kwamba ndicho kikwazo katika sekta ya elimu. Tukubali kwamba hich ni miongoni mwa vikwazo ila pia hata jamii ni kikwazo katika kuwatia moyo watoto kupata elimu.

Mwanafunzi mwenye viatu hivyo hapo juu; anajifikiriaje tangu anatoka nyumbani hadi anafika shuleni? Jamii inapaswa kutoa kila aina ya msaada kwa wanafunzi wa aina hii ili kuwasaidia na kuwatia moyo katika kufikia ndoto zao katika elimu.



HALI DUNI ISIKUKATISHE TAMAA KATIKA ELIMU. HALI DUNI ISIKUKATISHE TAMAA KATIKA ELIMU. Reviewed by Unknown on October 07, 2017 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.