MAKUTUPA ZA MPWAPWA NA KONGWA ZASHIKA MKIA 2017

Na. MED News
Ni jambo la kushangaza kwa wawili hawa wenye majina yanayofanana kutoka katika Wilaya  mbili tofauti za Mkoa wa Dodoma kuwa na matokeo yanayofanana katika Mtihani wa darasa la saba 2017.

Wilaya ya Kongwa ni moja kati ya Wilaya za Mkoa wa Dodoma ambayo pia imepakana na Wilaya ya Mpwapwa katika Mkoa  wa Dodoma. Licha ya Wilaya hizi kuwa majirani, Katika Wilaya hizi kuna shule za Msingi zene majina yanayofanana. Hizi ni shule za MAKUTUPA ambazo zinapatikana katika Mamlaka tofauti za Kiwilaya na Kielimu. 

Shule ya Makutupa ya Wilaya ya Kongwa katika mitihani ya Darasa la Saba 2017 ilisajili watahiniwa 23 ambao walifanya mitihani hiyo. Watahiniwa hao katika alama za ufualu wa jumla walipata alama 63.8696  katika kundi lake kiwilaya kwa shule zenye wahitimu chini ya 40 na kushika nafasi ya Mwisho katika kundi hilo yani ni shule ya 36 kati ya shule 36 kiwilaya. 

Katika kundi la shule zenye wahitimu chini ya 40 kimkoa Makutupa ya Kongwa ilishika nafasi ya 282 kati ya shule 282 katika Mkoa wa Dodoma na nafasi ya 6791 kati ya shule 6839 za kundi hilo kitaifa.
Picha hii haihusiki na hii habari bali ni moja ya mazingira ya shule zetu
Shule ya Msingi ya Makutupa ya Wilaya ya Mpwapwa yenyewe imekuwa na matokeo yanayofanana na kwa kiasi na ile ya Kongwa kama ifuatavyo. Katika shule hii watahiniwa waliofanya mtihani walikuwa 71 ambapo alama za ufaulu zilikuwa 79.5915 katika kundi la shule zenye wanafunzi zaidi ya 40 na kushika nafasi 64 kati ya shule 64 za kundi hilo Kiwilaya. Kimkoa shule hii imeshika nafasi ya 439 kati ya shule 463 za Mkoa wa Dodoma na Kitaifa imeshika nafasi ya 9491 kati ya shule 9736.



MAKUTUPA ZA MPWAPWA NA KONGWA ZASHIKA MKIA 2017 MAKUTUPA ZA MPWAPWA NA KONGWA ZASHIKA MKIA 2017 Reviewed by Unknown on November 03, 2017 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.