Moja kati ya vichocheo rafiki vya ufaulu kwa wanafunzi wa ngazi zote za elimu ni mazingira rafiki ya kujifunzia na kufundishia katika shule zetu. Shule isiyo na mazingira hayo ni nadra sana wanafunzi kuyapenda mazingira wanayo jifunzia kadhalika kwa walimu kuyapenda mazingira wanayo fundishia.
Kilio cha muda mrefu kutoka kwa walimu, wanafunzi na jamii kuhusu miuondombinu isiyo ridhsha katika shule za msingi na sekondari nchini; bado hakija sikika vya kutosha na pande zote husika katika kuondoa tatizo hilo.
Uhaba wa vyumba vya madarasa, uhaba wa matundu ya vyoo na ubovyo wa vyoo vyenyewe katika baadh ya shule za msingi na sekondari ni moja kati ya vikwazo vikubwa kwa wanafunzi na walimu shuleni.
Upo uhusiano mkubwa sana kati ya mazingira ya kujifunzia na ufaulu kwa wanafunzi wote wa kike na wale wa kiume. Huduma isiyoridhilsha hasa ya maeneo ya kujisitiri inawanyima morali wanafunzi wote bila kujali jinsia. Mfano kama choo hakina matundu ya kutosha, hakina paa, hakina milango madhubuti ya kumhifadhi mtumiaji kwa wakati huo, hakina maji nk. Mtumiaji hawezi kuwa huru kukitumia.
Choo cha wanafunzi katika moja ya shule ya Sekondari iliyotembelewa na MED hivi karibuni. Picha na J. Paul- MED |
Mazingira ya choo cha aina hii pichani ni dhahiri kuwa hakimpi uhuru mtumiaji katika kukidhi mahitaji yake na haki yake ya faragha.
Walimu na wanafunzi wamekuwa na wakati mgumu katika kutatua changamoto ya miundombinu katika shule zao kutokana na shule kutokuwa na fedha za kutosha katika ukarabati au uanzishaji wa ujenzi mpya nk.
Baadhi ya walimu walioongea na MED wameeleza kuwa licha ya kuwa Serikali inajitahidi kupeleka fedha za maendeleo shuleni; bado fedha hizo hazikidhi mahitaji ya shule. Tatizo la jamii kukataa kuchangia maendeleo ya shule kwa madai ya "Elimu Bure" ni kikwazo kingine katika kuboresha Elimu kwenye maeneo mbalimbali nchini.
Jamii imekumbushwa kusaidiana na nia njema ya Serikali ya awamu ya tano ya kutoa Elimu Msingi bure kwa kushirikiana na uongozi wa shule katika kutatua baadhi ya changamoto zinazokwamisha maendeleo ya watoto wao kielimu. "Ni kweli Serikali imebeba mzigo wa kusomesha watoto wetu bila wazazi kuchangia kwa lazima; hata hivyo kama wazazi na jamii tuna wajibu wa kuunga mkono nia hii ya serikali kwa kujitolea kuboresha mazingira ya watoto wetu kujifunzia" Alisema mmoja wa maafisa wa MED.
Jamii haina budi kutambua kuwa ili kupata mafanikio katika elimu ni lazima jamii, wazazi, walimu, wanasiasa, viongozi wa ngazi mbalimbali pamoja na Serikali kuungana kwa pamoja katika kuweka mkakati na nia moja ya kuziwezesha shule kuwa na mazingira bora na rafiki kwa wananfunzi na walimu.

MIUNDOMBINU ISIYO RAFIKI NI KIKWAZO KATIKA UFAULU
Reviewed by Unknown
on
September 30, 2017
Rating:
![MIUNDOMBINU ISIYO RAFIKI NI KIKWAZO KATIKA UFAULU](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgd4AaItc4RFYqbyxBECdKYuDrA7E0_VVeHHHMSdlbXDKKOT6imi8ELAUPbmr4MhhsVYMu2m8KJzw7aeuF-04GN9jmblFXrJF-Z8BK5SJux_vejfkQ0bdfIr4J2GY3pFJwf0be_ibkwflrs/s72-c/With+Logo.jpg)
No comments: