PICHA ZA MATUKIO YA KUKABIDHIWA MSAADA WA MADAWATI SHULE YA MSINGI CHIDACHI


Na. MED News
Shule ya Msingi Chidachi ni miongoni mwa shule za Msingi za Serikali zinazofanya vizuri kitaaluma katika Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma. Wadau mbalimbali wamekuwa bega kwa bega na shule hii kuunga mkono juhudi za walimu, wazazi, wanafunzi na jamii ya Chidachi katika Kata ya Mkonze kuboboresha Elimu katika shule hiyo.

Taasisi ya The Mumtaz Foundation Orlando. FL. USA kupitia shule yake ya Dar-Ul_Muslimeen ya Dodoma; ilitoa msaada wa madawati kwa shule hii ikiwa ni mchango wake kwa wenye uhitaji katika kusaidia maendeleo ya Elimu nchini.

 Pichani Juu kutoka Kushoto ni Mlezi wa Shule ya Msingi Chidachi na Mkurugenzi Mtendaji  wa Shirika la Marafiki wa Elimu Dodoma Bw. Davis J. Makundi, akifuatiwa na Mwenyekiti wa Shule hiyo Bw. Benedicto Mgimwa; Mwakilishi wa Dar Ul Muslemeen (ambaye jina lake halikupatikana), anayefuatia ni Mwl. Mkuu wa Shule ya Msingi Chidachi Bi. Ashura Muhoji.

 Aliyesimama ni Mwl. Mkuu wa Chidachi Bi. Ashura A. Muhoji akitoa maelezo kwa viongozi na wageni waliofika katika makabidhiano ya madawati kutoka Dar Ul Muslemeen.

 Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Msingi Chidachi wakiimba wimbo wa shukrani kwa wawakilishi wa Dar Ul Muslemeen kutokana na msaada wa madawati walioutoa kwa shule hiyo.
 Mwenyekiti wa shule ya Chidachi Bw. Benedicto Mgimwa akitoa neno la shukrani kwa wageni.

 Kutoka kushoto ni Mwakilishi wa Ofisi ya Elimu Manispaa, Mwalimu Mkuu Chidachi na Mwakilishi wa The Mumtaz Foundation Orlando. Fl. USA

  Picha ya Pamoja baina ya wawakilishi wa Shule, wadau wa Shule, uongozi wa Serikali ya Mtaa na Kata ya Mkonze pamoja na wageni toka The Mumtaz Foundation Orlando Fl. USA

 Mwakilishi wa The Mumtaz Foundation Orlando Fl. USA na Mwl. Mkuu Chidachi wakifurahia madawati yaliyotolewa kwa lengo la kupunguza uhaba wa madawati katika shule hiyo.
Wageni mbalimbali na uongozi wa shule pamoja na wawakilishi wa The Mumtaz Foundation Orlando Fl. USA wakiwa kwenye moja ya chumba cha darasa wakiangalia madawati yaliyokabidhiwa katika shule ya Chidachi iliyoko kata ya Mkonze Manispaa ya Dodoma.
PICHA ZA MATUKIO YA KUKABIDHIWA MSAADA WA MADAWATI SHULE YA MSINGI CHIDACHI PICHA ZA MATUKIO YA KUKABIDHIWA MSAADA WA MADAWATI SHULE YA MSINGI CHIDACHI Reviewed by Unknown on November 18, 2017 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.