UTAJIRI WA SHIKA NI KAMA ABRAMOVICH!


Dk. Shika hashikiki!

Ni vigumu kuamini lakini hali ndivyo ilivyo baada ya kubainika kuwa Dk Louis Shika ambaye hivi karibuni alikumbwa na kashfa ya kushindwa kununua nyumba za Lugumi; ni tajiri mwenye ukwasi mkubwa wa fedha tofauti na ilivyodhaniwa awali.

Kwa maneno yake mwenyewe daktari huyo wa binadamu alisema kuwa yeye ni shabiki mkubwa wa Chelsea kwa kuwa mmiliki wa klabu hiyo, Roman Abramovich ni rafiki yake wa karibu na mara kadhaa walikuwa wakifanya mazungumzo ya hapa na pale akiwa huko Urusi.Amesema kwa kuwa yeye ni mmiliki wa kampuni ya masuala ya kilimo iliyoko Urusi; walikuwa wakikutana na Abramovich mara kwa mara katika mikutano ya viwanda hali ambayo ilimpa hamasa yakupenda michezo na kujikuta akiipenda Chelsea ambayo inamilikiwa na tajiri huyo.

“Mimi nilikuwa ninashughulika na masuala ya kilimo na yeye masuala ya mafuta. Sasa kule Urusi kuna kawaida ya makampuni kukutana" alisema Dk. Shika.

Katika hali ya kawaida makampuni yanayofanya shughuli mbalimbali hukutana kupeana uzoefu, kubadilishana nawazo na kuangalia njia za kutatua changamoto zinazowakabili katika uendeshaji wa shughuli zao.
Dk. Shika hivi sasa amekuwa gumzo kila kona ya Tanzania kutokana na ujasiri wake katika maisha ambapo alijiingiza katika mnada wa kununua nyumba zilizokuwa zikipigwa mnada n kampuni ya YONO  kutokana na deni la mabilioni ya fedha za kodi anazodiawa Bw. Lgumi na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). 


UTAJIRI WA SHIKA NI KAMA ABRAMOVICH! UTAJIRI WA SHIKA NI KAMA ABRAMOVICH! Reviewed by Unknown on November 19, 2017 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.